Upcoming Events

Get Upcoming News and find the latest news updates from bagamoyo. Get current stories, articles and detailed news coverage

For Business like BICRC wish to offer a lot, the days of uncertainty are over.  At least for the next few years.  The inauguration of this Business Centre will prove that.  The team has laid down major objectives.  BICRC  should be an a informations and communications hub.  It is passionate.  It summed up some major agenda at least last twelve months.  And  from what we can tell, this time we will be giving you all necessary informations regarding  mission on many social issues in Tourism, Navigation and Exposure.  You will be linked with major trustable tour companies. 



  Queridos todos,
Gestión de Bagamoyo Informaciones Comunicaciones y Centro de Recursos se complace en desear una maravillosa Navidad y Fin de año Prosperours 2014

Los clientes todos sus estima, diversiones, seguidores, parters, simpatizantes y público en general.
"En esta era de la información, la información que más cuenta, así que permanezca conectado"





Wazaramo: Kabila lenye sherehe lukuki, usipochangia, kushiriki unatengwa



Anasema: “Sherehe hii inamuimarisha mtoto aweze kujitambua akiwa katika siku zake na kuvaa nguo za heshima.”
Anaongeza kuwa, mafunzo hayo humjenga mtoto katika umri huo mbele ya watu hasa watu anao waheshimu na watoto wadogo na kutofanya mapenzi kabla ya kuelekezwa mila na desturi au  kuolewa.
“Taratibu hizi zilikuwa zinawafanya watoto wa Kizaramo wasikutane na wanaume hadi waelekezwe mila na desturi au kuolewa, tena mila ya Kizaramo hawamchezi ngoma mtoto mwenye ujauzito,” anasema Mwajabu.
Anabainisha kuwa, baada ya hapo mtoto huendelea na shule hadi akimaliza masomo yake ndipo huwekwa ndani na huko anaweza kuwekwa kwa miezi au miaka kutegemea uwezo wa wazazi walivyojioanga kwa sherehe.
“Msichana akiwa ndani anajisugua kwa mapumba ya mahindi (chachu),  bila ya kuoga. Hiyo inakuwa ndiyo maji yake ya kuoga, japo kuna wachache wanaoga, lakini wengine wanajisugua kwa mapumba bila ya kuoga na wanakuwa weupe wanang’aa na kuvutia watu,” anasema na kuongeza; “Baada ya kukaa miezi kadhaa au miaka, ndipo wana ndugu wanaitisha kikao na kujadiliana namna ya kugawana majukumu ya kufanya sherehe ikiwamo vifaa vya mwali, vyakula na ngoma.”
 Anaongeza kuwa uamuzi wa kikao hicho unategemea wazazi wa mhusika wamejipanga vipi, kwani sherehe ya ngoma ina gharama  kubwa.
“Suala la kupanga ngoma ya kumcheza mtoto hutegemea na mtoto na wazazi kwani, watoto wengi sasa wanasoma hivyo wazazi wengi hawapendi kuwaweka watoto siku nyingi ndani,” anasema.
“Sherehe za ngoma ya kumcheza mwali hupangwa ndani ya siku saba, lakini siku ambazo ngoma hupingwa na watu kula na kushereheka ni Jumatano hadi Jumapili hiyo ni kwa zamani, lakini sasa watu wengi hufanya sherehe kwa siku mbili kulingana na hali ya kipato cha wazazi husika,” anafafanua.
Anaendelea kusimulia kuwa, katika sherehe hii chakula kikuu huwa  ni wali au pilau, hivyo kutokana na hali ya maisha na gharama zilivyopanda, wengi hufupisha siku za sherehe.
 “Sherehe hiyo ya kucheza mwali huitwa Mkole  ambapo mtoto wa kike hufunzwa vitu vingi vya kimaisha ikiwamo namna ya kuishi na watu wa jamii yake na baada ya hapo hutolewa nje akiwa amepambwa kama bi harusi,” anasema Mwajabu.
Anasema kuwa katika kumtoa mwali anaweza akatolewa kwa muziki, ngoma ya kienyeji au kwa Maulidi na hapo ndugu na jamaa hukusanyika na kumpa zawadi.
“Katika ugawaji wa  zawadi hizo mtoto wa kike hupewa zawadi nyingi kuliko wa kiume. Hupewa zawadi ya nguo mbalimbali , kitanda , godoro vyombo vya nyumbani, vito vya dhahabu, meza za vyakula, mazuria, friji, jiko la umeme ,feni na vingine,” anasema Mwajabu.